September 17, 2014


Mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, amefunguka na kumwambia kocha wake, Mzambia, Patrick Phiri, kuwa nafasi yoyote atakayompanga uwanjani atahakikisha anafunga tu, hivyo asipate taabu kujiuliza mara mbilimbili kuwa anafaa kucheza nafasi gani hasa kati ya winga na straika.

Kauli hiyo ya Okwi inakuja baada ya kuwepo kwa baadhi ya maoni kwa wadau kuwa, mshambuliaji huyo ameshindwa kufumania nyavu ndani ya mechi tatu za kirafiki za hivi karibuni kwa kuwa anapangwa kama namba tisa, kitu ambacho Okwi amekipinga na kutoa msimamo wake huo.

Okwi amesema kuwa yeye ni mshambuliaji mwenye uwezo wa juu na huwa haangalii anacheza wapi ili aweze kufunga kwa kuwa anajua suala hilo ni jukumu lake, kwa hiyo atafunga tu bila ya kujalisha kama anacheza kiungo, winga au mshambuliaji wa kati.

“Huku kutokufunga kwenye mechi za hivi karibuni, imetokea bahati mbaya tu lakini si kwamba eti nashindwa kufunga kwa kuwa nacheza mshambuliaji wa kati, kocha anaweza kunipanga kokote pale anapopenda yeye na mimi nikafanya kazi yangu kama kawaida wala haina shida.
 “Mimi kazi yangu hasa ni kufunga na kuisaidia timu kupata ushindi na naweza kuyafanya hayo hata nikicheza kiungo, winga au mshambuliaji, kwa hiyo ni kocha mwenyewe atakapoona nafaa, akinipanga mimi nitafanya kazi yangu,” alisema Okwi.

Tangu Okwi atue Simba hivi karibuni akitokea Yanga, tayari ameshacheza mechi tatu za kirafiki lakini zote hakuna aliyobahatika kutikisa nyavu. Mechi hizo ni dhidi ya Gor Mahia ya Kenya waliyoshinda mabao 3-0, kisha URA ya Uganda waliyofungwa 1-0 kabla ya kuwavaa Ndanda wikiendi iliyopita na kutokananao suluhu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic