September 22, 2014


Uongozi wa klabu ya Simba umesema sare ya mabao 2-2 dhidi ya Coastal Union, jana, haukuwa mzuri kwao lakini wameupokea kama changamoto.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema wanaichukulia sare hiyo kama changamoto na sehemu ya kujipanga.
KABURU.
“Hakuna aliyetarajia, inawezekana vijana wetu walijisahau baada ya kuongoza kwa mabao mawili wakaona tumeshinda.
“Kipindi cha pili Coastal Union wakajirekebisha na kucheza mchezo mzuri na kutupa wakati mgumu, mwisho wakasawazisha,” alisema Kaburu.
“Tayari tumeanza kambi Zanzibar na tutayatumia makosa ya mechi iliyopita kama sehemu kujiimarisha.”

Simba itacheza mechi ya pili dhidi ya Polisi Morogoro katika mechi itakayopigwa Jumamosi ijayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic