September 22, 2014


Mashabiki wa soka nchini Ureno wamechangia kwenye mitandao mbalimbali wakionyesha kusikitishwa na ugomvi wa nyota wao wawili.

Kocha Jose Mourinho wa Chelsea na mshambulia Cristiano Ronaldo wa Real Madrid wameeleza hadharani kuwa hawana urafiki tena.
Mashabiki hao wa soka wameeleza wazi kusikitishwa na hali hiyo huku wakishindwa kugawanyika wampede nani.
Baadhi wamesema Ureno yenye watu milioni 11 na nyota wachache wanaojulikana zaidi duniani kama hao wawili, hivyo hawakupaswa kuwa maadui.
Kauli ya Mourinho kwamba walitolewa kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2012 baada ya Ronaldo kukosa penalti na limekuwa jambo ambalo linamuumiza kila mara ilioonyesha kumuudhi mshambuliaji huyo.
Ronaldo alijibu mashambulizi kwa kusema hayuko katika soka kutafuta marafiki na hiyo ilikuwa baada ya kuulizwa kama uhusiano wake na Mourinho ni mzuri.
Wawili hao walifanya kazi pamoja Real Madrid tokea mwaka 2010 hadi 2012 Mourinho alipoondoka na kwa mambo yanavyokwenda inaonekana uhusiano wao haupo.
“Urafiki wetu haupo, ulishakufa, si lahisi kutuona tukiwa pamoja,” Mourinho aliiambia moja ya runinga marufu ya Ureno wakati akifanyiwa mahojiano.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic