September 18, 2014


Zinedine Zidane huenda akafungikiwa kufundisha soka barani Ulaya kwa miezi sita.
Kwa sasa ni Kocha Mkuu wa Real Madrid, kikosi B, lakini ana kesi.

Kesi yake ni madai kwamba hana vigezo vinavyompa leseni ya kufundisha katika daraja hilo.
Chama cha Makocha cha Hispania (CENAFE), kimeamsha madai kuhusiana na Zidane na kusisitiza kinataka kupata uhakika.
Iwapo itabainika kwamba Zidane hana vigezo sahihi, maana yake Real Madrid itakuwa imekiuka kipengele namna 104 na adhabu yake ni kufungiwa kuanzia mechi nne hadi 16 au mwezi mmoja hadi sita.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic