October 27, 2014

YANGA WAKIJIFUA MJINI KAHAMA, LEO.
Kikosi cha Ambassador cha mjini Kahama kitakuwa mwenyeji wa Yanga katika mechi ya kirafiki itakayopigwa Jumatano.

Yanga iko katika maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar itakayopigwa wikiendi hii kwenye Dimba la Kaitaba,mjini Bukoba.

Mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Kahama.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto ameiambia SALEHJEMBE kuwa kweli mchezo huo utakuwepo.
“Ni kweli tuna mechi, itapigwa Jumatano na baada ya hapo ndiyo tutasafiri kwenda Bukoba, hiyo timu inashiriki daraja la pili,” alisema Kizuguto.

Mechi hiyo itakuwa ya pili ya Yanga kirafiki kwa kuwa ilianza kucheza na CDA ikiwa mjini Dodoma na kutoka nayo sare ya bila kufungana halafu ikasafiri hadi Shinyanga na kuifunga Stand United kwa mabao 2-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic