October 24, 2014


Baada ya kipa wa zamani wa Barcelona kugoma kufanya majaribio Liverpool, sasa Manchester United imeanza mazungumzo naye ili ikiwezekana atue Old Trafford.


Victor Valdes ,32, aligoma kufanya majaribio ya siku nne kama Liverpool walivyokuwa wametaka.
Lakini Man United kupitia kocha wake, Louis van Gaal wameanza naye mazungumzo.
Kipa huyo aliyechwa na Barcelona sasa yuko huru hivyo haitakuwa gharama kubwa kumpata.

Na kama atakubali kujiunga na Man United, timu ya tiba ya klabu hiyo ndiyo itaendelea kumsimamia hadi atakapokuwa fiti kiafya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic