October 31, 2014


31 Oktoba 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Kampuni ya Mawakili ya MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, ambayo inawakilisha vilabu 13 vya LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA, inapenda kutoa tamko kwa umma kama ifuatavyo:

1.          Kampuni ya MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, iliteuliwa na vilabu 13 vya LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA, kwa maandishi, ili kuwawakilisha na kuwatetea katika kudai haki zao ambazo tayari SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF) liliamua kukata fedha za udhamini na viingilio vya mechi pasipo kuwashirikisha. Dk. Damas Daniel Ndumbaro, wakili mwandamizi, ndiye aliyekabidhiwa file hilo kwa mujibu wa utaratibu wa ofisi yetu.
2.          Kwamba, tarehe MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, kupitia wakili wake mwandamizi, Dk. Damas Daniel Ndumbaro, iliandika barua ya madai (Demand Notice) TFF na kuongea na waandishi wa habari.
3.          Kwamba tarehe Mheshimiwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Juma Nkamia (MB) aliitisha mkutano kati ya TFF (ambayo iliwakilishwa na Wilfred Kidau-Mjumbe Kamati ya Utendaji, na Selestine Mwesiga, Katibu Mkuu), Bodi ya Ligi, Vilabu vya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania na Dk. Damas Daniel Ndumbaro (kama wakili wa vilabu). Mwenyekiti wa Mkutano huo, Mh. Juma Nkamia alitoa fursa kwa TFF, Bodi ya Ligi, na Wakili wa vilabu kutoa maelezo yao na hatimaye  Mh. Juma Nkamia alitoa maelekezo kama ifuatavyo:
i.             Jamal Malinzi sio Rais wa Nchi, na aliwaagiza wawakilishi wa TFF wafikishe ujumbe huo kwa Bw. Jamal Malinzi.
ii.          Makato ya Tshs. 1000/= kwa kila tiketi ni wizi wa mchana.
iii.       TFF isitishe makato ya 5% na Tshs. 1000 kwa kila tiketi mpaka watakapoongea na kukubaliana na vilabu
4.          Baadaya hapo, MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, ilikutana na vilabu ambayo vilikuwepo siku hiyo na kukubaliana kuwa sasa tusibiri majadiliano na TFF na kwamba MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, ikiongozwa na Dk. Ndumbaro iandae mapendekezo ili yajadiliwe na mkutano mkuu wa vilabu.
5.          Kwamba tarehe 11 Oktoba 2014 TFF ilifanya mkutano wa Kamati ya Utendaji na kutoa tamko kuwa kumekuwa na taarifa za upotoshaji kuhusu kanuni za ligi kuu na kwamba Sekretariati ya TFF imefungua mashtaka dhidi ya Dk. Ndumbaro ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba.
6.          Kwamba Kamati ya Utendaji ya TFF iliendelea kusema kuwa Kutokana na madai ya klabu kuhusu vipengele kadhaa vya Kanuni za Ligi Kuu 2014/15, Kamati ya Utendaji imepanga kukutana na viongozi wa klabu za Ligi Kuu siku ya Jumamosi, Oktoba 18 mwaka huu ili kuwasikiliza na kushauriana kuhusu changamoto za kikanuni na uendeshaji wa mashindano kwa ujumla na kwamba.
7.          TFF imefanya kosa kumshitaki Dk. Ndumbaro kwa kofia ya Mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Simba kwasababu barua toka MALETA & NDUMBARO ADVOCATES, barua za vilabu 13 na taarifa kwa vyombo vya habari ilikuwa bayana kuwa Dk. Ndumbaro anawakilisha vilabu vya ligi kuu kama wakili toka kampuni ya MALETA & NDUMBARO ADVOCATES na wala sio mwakilishi wa Bodi au Mwenyekiti wa uchaguzi wa Simba kwasababu hakukuwa na uchaguzi wa Simba.
8.          Kwamba TFF inakiri kuwa klabu za Ligi kuu zinapaswa kukutana na TFF kujadili kasoro za Kanuni za Ligi kuu. Hapa TFF inakiri kuwa haikukutana na vilabu katika mchakato wa kutunga kanuni hizi na kwamba kanuni hizo zinakasoro. Ifahamike kwamba hayo ndio madai ambayo vilabu kupitia MALETA & NDUMBARO ADVOCATES iliyapeleka TFF kwa maandishi.
9.          Tarehe 7 Oktoba 2014 TFF iliepeleka Mshtaka katika Kamati ya Nidhamu dhidi ya Dk. Ndumbaro. Kamati ya Nidhamu ilipanga kusikiliza Mashtaka hayo tare 09 / 10 / 2014 saa 08: oo mchana, yaani siku mbili tu baadaya ya kuwasilishwa katika kamati ya nidhamu. Mashitaka hayo yalijaa ubabaishaji na chuki binafsi dhidi ya wakili wa vilabu 13 vya Ligi Kuu.
10.     Kwamba TFF ililazimisha kusikiliza mashtaka hayo kwa haraka na dharura ya ajabu pasipo kuwepo Dk. Ndumbaro ambaye alitoa taarifa ya maandishi kuwa atakuwa safarini Nchini Marekani kikazi, kwa barua ya tarehe  8th October 2014.
11.     Kwamba Kamati ya Nidhamu ya TFF ilitoa maamuzi ya kumfungia Dk. Ndumbaro asijihusishe na Soka kwa kipindi cha miaka saba pasipo kutoa sababu za msingi za kufanya hivyo wala kutoa nakala ya hukumu hiyo.
12.     Kwamba MALETA & NDUMBARO ADVOCATES kwa niaba ya vilabu vya Ligi kuu inapinga adhabu hiyo ya uonevu kwa misingi ifuatayo:
i.             Kamati ya nidhamu ya TFF haina mamlaka ya kisheria ya kushughulikia suala hili. (ARTICLE 2, 3,76 and 77 of TFF Disciplinary  Code)
ii.          Kamati ya nidhamu ya TFF ilikosea kuamua suala hili bila kutoa haki ya msingi ya kuisikiliza MALETA & NDUMBARO ADVOCATES na Dk. Damas Daniel Ndumbaro
iii.       Hakuna Chombo chochote cha TFF chenye mamlaka ya kumzuia au kumfungia Wakili wa kujitegemea kuwawakilisha wateja wake.

13.     MALETA & NDUMBARO ADVOCATES inaandaa kesi ya madai dhidi ya TFF kwa kuizuia isifanye biashara yake halali.
14.     MALETA & NDUMBARO ADVOCATES inapenda kuwajulisha wadau wote kuwa kupinga maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya TFF sio kosa. Ikumbukwe kuwa JAMAL MALINZI aliwahi kupinga maamuzi ya FIFA, CAF na TFF kuhusu mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2013, kwa njia ya Circular Resolution, ili kuunda Kamati za Rufaa ya Uchaguzi, Kamati ya Maadili na Club Lincensing. Lakini leo Jamal Malinzi hataki kupingwa huyu ni dikteta.
15.     Kwamba MALETA & NDUMBARO ADVOCATES inaandaa mashtaka dhidi ya Uongozi wa TFF, katika mambo yafuatayo:
i.             Ubadhirifu wa US$ 200,000 fedha za TBL udhamini wa Taifa Stars
ii.          Kupinga Maamuzi ya FIFA kurejea Karume ( Haya yalikuwa mapendekezo haikuwa amri)
iii.       Kufanya matumizi na manunuzi bila kibali cha kamati ya fedha ambayo ndiyo kamati ya manunuzi ya TFF kwa mujibu wa kanuni za manunuzi za TFF, manunuzi yaliyofanyika yanahusiana na Vifaa vya michezo wakati wa maboresho ya Taifa stars, Tiketi za ndege za Taifa Stars, timu ya wanawake na za vijana katika michezo yake na hotel za kambi ya timu ya Taifa ambapo hakukuwa na tenda zilizotangazwa wala ushindanishwaji wa aina yoyote jambo linaloashiria matumizi mabaya ya madaraka na fedha na kwa kuwa Rais ndiye msimamizi wa shughuli za sekretariet kikatiba jambo hili linakuwa pamoja na mengine ni suala la kimaadili kwa sheria za mpira.

16.     Kwamba  MALETA& NDUMBARO ADVOCATES inaandaa mashtaka dhidi ya Jamal Malinzi kwa Kupinga Maamuzi ya FIFA, CAF na TFF ili kufanya marekebisho ya Katiba mwaka 2013.
17.     Tarehe  21 Oktoba 2014, Dk. Damas Daniel Ndumbaro alikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya TFF lakini mpaka sasa Kamati ya Rufaa ya Nidhamu TFF haijasema lina inakaa. Tunatarajia kuwa haraka na dharura iliyotumika katika kuamua shauri katika kamati ya nidhamu itatumika pia kuamua shauri katika rufaa. Leo ni siku ya 10 toka rufaa ikatwe lakini bado kimya wakati ilichukua siku 2 tu kusikiliza kesi ya msingi.
KWAHIYO Dk. Damas Daniel Ndumbaro wa MALETA & NDUMBARO ADVOCATES kwa naiba ya wateja wetu tunasema kuwa:

a.           Tutaendelea na kuwawakilisha wateja wetu kwa uadilifu wa hali ya juu.
b.           Kwamba madai yote tuliyoyasema katika barua ya awali dhidi ya TFF ikiwemo madai yanayohusiana na Mkutano Mkuu yapo pale pale.
c.           Tumekata Rufaa dhidi ya maamuzi ya kamati ya nidhamu ya TFF kuanzia tarehe 21 Okotba 2014
d.          Tunaandaa mashtaka dhidi ya Uongozi wa TFF kwa ubadhirifu wa fedha za umma
e.           Tunaandaa mashtaka dhidi ya TFF kwa kosa la kupinga agizo la FIFA kurejea Karume
f.             Tunaandaa Mashtaka dhidi ya Jamal Malinzi kwa kosa la kupinga Maamuzi ya TFF, CAF na FIFA katika mabadiliko ya Katiba ya TFF mwaka
2013.
Wako

Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
For: Maleta & Ndumbaro Advocates
www.maletandumbaroadvocates.com

Nakala:        i. Vilabu 13 vya Ligi Kuu
ii. Mh. Naibu Waziri
              Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Description: Sign(Letter head).png


1 COMMENTS:

  1. inamaa ndimbalo adv. ndio inamiliki wapenda mpira wote tanzania au make mengine ya si kwake bali anayabeba kama ndio baba mzazi wa mpira tanzania hapa kuna ulaji mmoja hakinyimwa ndio kelele swala la vilabu its ok lakin haya mengine tusubiri upande wa pili make yy si mwasibu wa Tff wala mtunza fedha wa Tff sasa kapuni yake inataka kujitangaze kupitia Tff au thing twice

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic