October 21, 2014


Kiungo Maroaune Fellaini ambaye amekuwa hakubaliki katika kikosi cha Man United, leo amefunga bao safi kabisa na kuisaidia Man United kuamka katika sare yake ya mabao 2-2 dhidi ya wenyeji wake Wes Brom.

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England, katika dakika ya 48, Fellaini alifunga bao akiwa ndiyo anagusa mpira wake wa kwanza baada ya kuingia akitokea benchi katika kipindi cha pili. Kabla ya kufunga aliweka mpira gambani, akadanganya kabla ya kupiga shuti kali.

Bao hilo lilikuwa la kusawazisha baada ya Stephane Sessegnon aliyekuja nchini na timu yake ya taifa ya Benin iliyochapwa na Stars bao 4-0, kuanza kuipatia Wes Brom bao safi. Bao lake alilifunga katika dakika ya 8 tu.
Fellaini aliendelea kufanya vizuri katika kiungo hata baada ya Barahino kufunga bao la pili akiwatoka mabeki wa Man United waliojichanganya katika kuweka mtego wa offside.

Bao hilo la Berahino katika dakika ya 66, halikuikatisha tamaa Man United iliyoendelea kupambana hadi dakika ya 87 ilipopata bao hilo kupitia Blind aliyepiga mkwaju mkali baada ya Falcao kumpa pasi.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic