October 31, 2014


Ishu ya kipa wa Yanga, Juma Kaseja na klabu yake limechukua sura mpya baada ya uongozi wa Yanga kutoa kauli kali juu ya aliyejitambulisha kuwa ni meneja wa kipa huyo, huku ikielezwa kuwa kipa huyo amepata ofa ya kucheza soka Uarabuni.


Meneja wa Kaseja, mwanamichezo Abdulfatah Saleh ambaye amejitambulisha kuwa ni meneja wa mchezaji huyo, amenukuliwa na vyombo vya habari likiwemo gazeti hili, akisema kuwa Yanga imevunja mkataba na mteja wake kutokana na kukiuka masharti ya mkataba.

Akijibu madai hayo, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, amesema kuwa, kisheria wao hawamtambui huyo anayejiita meneja wa Kaseja na hivyo hawawezi kutambua madai ya kuvunjwa kwa mkataba kama inavyoelezwa.

Njovu alikataa kujibu swali la mkataba huo kwa njia ya simu na kuomba atumiwe barua pepe, alipoulizwa kupitia barua pepe, alijibu kwa kifupi kama ifuatavyo:

“Siwezi kukujibu maana mchezaji Juma Kaseja hana meneja anayetambulika na taasisi yoyote, iwe Yanga, TFF au hata Fifa.”

Kisha baada ya hapo akaambatanisha na majina ya mawakala ambao wanatambulika Fifa, akiwataja kuwa ni Ahmed Binkleb, John Ndumbaro, Mehdi Remtulla na Ally Saleh.

Wakati hayo yakiendelea, Abdulfatah Saleh ameliambia gazeti hili kuwa Kaseja anaendelea kupata ofa mbalimbali ikiwemo kutoka Dubai.

“Kaseja kubaki Yanga baada ya mzunguko huu wa sasa ni mgumu kutokana na Yanga kukiuka masharti ya mkataba kwa kushindwa kumalizia fedha za usajili zilizobaki, shilingi milioni 20, ambazo zilitakiwa zilipwe kabla ya Januari 15, mwaka huu.

“Kuna klabu mbili za Dubai lakini bado mazungumzo yanaendelea,” alisema Abdulfatah.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic