October 18, 2014



MPIRA UMEKWISHAAA;;;; Dk 90+4 (Chanongo anafanyiwa madhambi, Simba wanapata faulo, anapiga Kisiga....njeeee)

Dk 88,Yanga inapata kona ya nne, lakini haina matunda.

Dk 87, mpira wa kurusha wa Twite unatua kichwani kwa Cannavaro, lakini kidogo tu, unatoka pembeni ya lango la Simba.


Dk 84, Chanongo anawachambua mabeki wa Yanga, lakini shuti lake linapaa juuuuuuu...

Dk 82, Yanga inamtoa Jaja, nafasi yake inachukuliwa Hamisi Kiiza

Dk 80, Hadi sasa Yanga imepata kona 3, halikadhalika Simba 3

Dk 79, Okwi anaingia eneo la hatari lakini mabeki wa Yanga wanaokoa na kuwa kona, anaichonga lakini haina matunda.
Dk 77, Manyika anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Coutinho aliyekuwa peke yake akimtazama.


Dk 75 Coutinho anapewa pasi nzuri kutoka kwa Jaja, lakini anashindwa kuifanyia kazi


Dk 74, Okwi analambwa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Juma Abdul.
Dk 73, Jaja yeye na Manyika, lakini napiga mpira mkubwaaa....

Dk 72, Ngassa anaingia ndani ya eneo la hatari baada ya kupokea pasi safi ya Coutinho, lakini Manyika anatoka na kuuwahi.Dk 68, Yanga wanamtoa Niyonzima na nafasi yake inachukuliwa na Simon Msuva
Dk 67,  Chanongo anapiga mpira unagonga mwamba, hata hivyo mwamuzi anasema kablaya kupiga alikuwa ameotea.

Dk 64, Mkude anatolewa uwanjani kabisa, taarifa zinaeleza amekimbizwa hospitali kutokana na kuteguka bega.
Dk 61, Pierre Kwizera raia wa Burundi anaingia kuchukua nafasi ya Mkude

Dk 60, Kiemba anapiga kichwa safi lakini kidogo tu linatoka.
Dk 54, Mkude anaumia na kutolewa nje....
Dk 47, Okwi anapiga shuti kali lakini linawababatiza mabeki

MAPUMZIKO:
Dk 45+1, Ngassa, Hassan Isihaka wanalambwa kadi ya Njano, baada ya Ngassa kumkita Isihaka ikiwa ni maa ya pili kucheza rafu hiyo. Lakini Isihaka anapata adhabu kutokana na kumsukuma Ngassa.


Dk 38, Simba wanamtoa Ndemla na nafasi yake inachukuliwa na Shabani Kisiga
Dk 31, Okwi anaingia ndanilakini Dida anadanya kazi ya ziada kuokoa hatari.


Dk 29, Yanga wanapata kona lakini kichwa na Oscar hakikulenga lango
Dk 20, Coutinho anagongana na Kiemba, anatolewa nje kutibia baada ya kuchanika, lakini anarudi uwanjani


Dk 18, Okwi anatuliza kifuani mbele ya Juma Abdul, anaingia vizuri mbele ya Cannavaro na kupiga shuti kali, linatoka juu kidogo tu ya lango la Yanga...ilikuwa hatari.

Dk 17:36, Coutinho anapiga shuti lakini Manyika anatoka na kulidaka vema.

Dk 17 Okwi anatengenezewa na Shabalaka anapiga shuti kali linatoka nje kidogo.
Dk 13, Jaja anatuliza mpira katikati ya mabeki ya Simba na kuupira kiufundi, lakini Manyika anashituka na kuudaka.

Dk 6, Jaja anapiga kichwa lakini kinatoka nje kidogo ya lango la Simba.
Dk 4 Okwi anaingia na kujaribu lakini shuti lake linakuwa nyanya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic