October 24, 2014


Jumla ya wanachama na mashabiki 35 wa Klabu ya Yanga kutoka matawi ya Tandale Kwa-Mtogole na Mpira Akili, wametenga shilingi milioni mbili kwa ajili ya kuifuata timu yao mkoani Shinyanga katika mchezo dhidi ya Stand United.


Katibu wa Tawi la Mpira Akili, Abass Ngau, ameliambia Championi Ijumaa, jana kuwa walitarajia kuondoka leo Ijumaa alfajiri kwenda Shinyanga ambapo amesema huo ndiyo utaratibu waliojiwekea kwa ajili ya kuipa sapoti timu yao ambayo ina nyota kadhaa akiwemo Mbrazili Andrey Coutinho.

“Tupo kama watu 35 na kila mmoja amechanga shilingi 70,000, huo ni utaratibu ambao tumejiwekea ili kuongeza hamasa kwa timu yetu na pia watu wa Tawi la Tandale wametuunga mkono,” alisema Abass.

Yanga itakuwa mgeni wa Stand, kesho Jumamosi katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic