October 1, 2014

MILOVAN.
Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic amewataja wachezaji wa zamani wa klabu hiyo kuwa ni sehemu ya historia ya mafanikio yake.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, Milovan amewataja wachezaji kadhaa ambao ni Haruna Moshi ‘Boban’, Shomari Kapombe ambaye sasa yuko Simba, Felix Sunzu, Juma Nyosso, Amir Maftah na Emmanuel Okwi ambaye amerejea Simba.
Milovan ambaye sasa ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Mnyammar ameweka picha za wachezaji hao pamoja na kombe na kusema ni jambo lisilosahaulika.
Alipoulizwa na gazeti hili kwamba alikuwa na maana gani kutupia picha za wachezaji hao, alisema.
“Kilikuwa kipindi ambacho ni Simba itakayokubukwa kila wakati, walikuwa wachezaji hodari na waliocheza kwa mapenzi makubwa.
“Unakmbuka, Simba ya kipindi kile ilikuwa ni Simba bora na yenye uwezo wa kupambana. Bado ninapakumbuka Tanzania, ninapapenda sana,” alisema Milovan.
Katika wachezaji wote aliowataka ni mmoja tu, Okwi ambaye tena amerejea Simba baada ya kwenda Tunisia, baadaye akarejea kwao Uganda, halafu akarudi Tanzania na kujiunga na Yanga kabla ya kurudi ‘kwao’ Simba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic