October 21, 2014


Ronaldo ndiye mshambuliaji mwenye kasi zaidi ya kupachika mabao kwa maana ya wastani.

Hadi sasa ana wastani wa kufunga bao katika kila dakika 42 alizoichezea Real Madrid kwenye la Liga.
Anafuatiwa na Neymar ambaye amecheza msimu mmoja wa La Liga na huu ni wa pili akiwa na Barcelona.
Neymar ana wastani wa kufunga bao katika kila dakika 52 alizoichezea Barca.
Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi anaonekana kutokuwa na bahati ya kutosha.
Kwani ana wastani wa dakika 102 ili kupata bao moja.
Maana yake hana uhakika wa kupata bao katika dakika 90 za mchezo mmoja. Anaweza kufunga au la.
Tayari wachambuzi wa soka nchini Hispania wanaeleza huenda Messi atakuwa na mabao kiduchu zaidi, lakini atafanya vizuri zaidi kwenye pasi zinazozaa mabao yaani asisti.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic