October 2, 2014


Kamati ya utendaji ya TFF ilimteua Leodeger Chilla Tenga kuwa mwenyekiti wa kwanza wa mfuko wa maendeleo ya soka nchini.


huu na wajumbe wake ni Bw Tarimba Abbas, Ephraim Mafuru, Mzee Ayoub Chamshama,   Frederick Mwakalebela na  Zarina Madabida. Bw Henry Tandau na Bw Boniface Wambura ni waratibu wa mfuko huu. Imani ya TFF ni kuwa wajumbe hawa kwa kutumia uzoefu wao katika uongozi wa jamii watatusaidia kuhakikisha mfuko huu unaanza vyema shughuli zake.
Upande wa TFF tumefungua akaunti maalum benki kwa ajili ya kuingiza fedha zote zinazokusanywa kama mchango wa TFF kwenye mfuko huu zikiwemo asilimia 5 za makato ya fedha za udhamini na ZILE zitokanazo na mfuko wa jichangie,TFF inatoa wito kwa wadau wote wa mpira wa miguu Tanzania kuchangia mfuko huu ili utumike kunusuru mpira wetu. Fedha zitakazokusanywa matumizi yake yatasimamiwa na kanuni za uendeshwaji wa mfuko huu.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic