October 23, 2014

MTIBWA SUGAR.
Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema wanakwenda Mbeya kwenda kupeleka mauaji mjini Mbeya.

Kifaru amesema wataitwanga Mbeya City kwao Mbeya kwenye mechi ya Jumapili na kuondoka na pointi tatu.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Kifaru alisema wamejiandaa vizuri na Mbeya City wasubiri kipigo cha pili baada ya kile cha Azam FC.
“Sisi tuko tayari, kikosi kizima kimeanza safari ya Mbeya kwa ajili ya kupeleka mauaji hayo.
“Tutawafunga na kuendeleza kubeba pointi tatu halafu tuondoke kwa mbwembwe,” alijigamba Kifaru.

Tayari Mbeya City imeishapoteza mchezo nyumbani kwao Mbeya baada ya kuchapwa kwa bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic