October 25, 2014

TAMBWE AKIPAMBANA UWANJANI...

Kiungo Shabani Kisiga ma Mrundi Amissi Tambwe ndiyo wataoongoza mashambulizi ya Simba leo mjini Mbeya dhidi ya Prisons.

Simba ambayo iko ugenini Mbeya, iko tayari kupambana katika mechi yake ya kwana ya ugenini.
Pia inapambana ikitaka ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi nne nyumbani Dar na kutoka sare zote.
Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri, amesema Tambwe ataanza au atapewa nafasi kubwa ya kucheza.
Pia kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’ ana nafasi kubwa ya kuanza katika kikosi cha leo.
Tayari mashabiki wameanza kusogea kwenye eneo la Uwanja wa Sokoine kwa ajili ya mechi hiyo.

Simba inakuwa timu kubwa ya kwanza kucheza Mbeya tokea kuanza kwa msimu huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic