October 20, 2014


Kama mshambuliaji wa Yanga, Geilson Santos Santana ‘Jaja’ na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Andrey Coutinho ambao ni raia wa Brazil wangetumia vyema nafasi walizozipata kufunga mabao, basi uongozi wa timu hiyo ungetoa shilingi milioni 80 kwao.

Wabrazili hao walikosa nafasi hizo za wazi wakati timu yao ilipovaana na wapinzani wao, Simba, katika mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo ilimalizika kwa suluhu.

Jaja na Coutinho walikosa mabao hayo wakiwa wamebaki wao na kipa ndani ya sita wakishindwa kumfunga kipa chipukizi, Peter Manyika Jr.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo, wachezaji hao kabla ya mechi hiyo waliahidiwa kupewa fedha hizo kama morali endapo watawafunga watani wao wa jadi Simba.

Chanzo hicho kilisema, fedha hizo waliahidiwa siku moja kabla ya mechi wakati viongozi walipoitembelea kambi ya timu hiyo iliyoweka Landmark, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

 “Wachezaji wameikosa ahadi waliyopewa na viongozi wao, kabla ya mechi na Simba viongozi walikwenda kambini Mbezi Beach kwa ajili ya kwenda kuwatembea pamoja na kula chakula cha usiku.


“Waliahidiwa kupewa mil. 80 zilizopangwa kugawanywa kwa kuanzia kwa wachezaji na benchi zima la ufundi,” kilisema chanzo hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic