November 24, 2014

MKURUGENZI MTENDAJI WA AZAM TV, RHYS TORRINGTON (KULIA) AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Azam Media leo imezindua promosheni ya Mtonyo Chap Chap kwa wateja wake wa rekoda zao kwenye makao ya makuu ya ofisi zake zilizopo Tazara, jijini Dar es Salaam.


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja Mauzo na Masoko wa Azam Media, Mgope Kiwanga alisema promosheni hiyo ya mwezi mmoja iliyoanza leo (jana) na kumalizika Desemba 31, mwaka huu.

“Leo (jana) tumezindua promosheni kwa wateja wetu, hiyo yote katika kusherehekea kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Azam TV, hivyo katika kusherehekea tumeona ni vyema tukasherehekea na wateja wetu kwa kuanzisha promosheni hiyo.

“Kila wiki tunatoa washindi watakaopatikana kwa kuchezesha droo kwa wateja wetu wa zamani na sasa, washindi watajinyakulia fedha taslimu shilingi 165,000 bei ambayo ya kufunga Azam TV,”alisema Kiwanga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic