November 29, 2014

 Kiungo nyota wa Manchester United, Angel Di maria ameeleza machungu yake ya kutocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na kusema, kamwe huwa haangalii mechi hizo.


Di Maria ambaye ni mchezaji ghali zaidi England amesema wakati wa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya, amekuwa akiutumia muda huo kucheza na mwanaye.

Hata hivyo, winga huyo aliyesajiliwa kwa pauni milioni 60 akitokea Real Madrid, anaamini Man United itarejea kwenye michuano hiyo msimu ujao.

Man United bado imekuwa inakwenda kwa muda wa kusuasua kutokana na kutopata matokeo mazuri kwenye Ligi kuu England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic