November 27, 2014


Kiungo Mbrazil, Emerson Roque leo ameanza kujifua katika kikosi cha Yanga.
Imeelezwa atafanya majaribio kwa wiki mbili, leo imekuwa siku ya kwanza.

Katika mazoezi hayo ya Yanga kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam kulikuwa na ulinzi mkali.

Emerson ambaye inaelezwa atachukua nafasi ya mshambuliaji, Jaja alionekana kama vile amezoeana na wachezaji wengine wa Yanga.


Pamoja naye, kiungo Coutinho na Kocha Marcio Maximo, nao walianza mazoezi yao kwa mara ya kwanza baada ya kurejea nchini, jana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic