November 24, 2014


Mshambuliaji wa Yanga, Mbrazil, Geilson Santos ‘Jaja’ aliwaaga wachezaji wake kabla ya kurudi kwao Brazili kwa kuwaambia kwamba hatarejea tena kuichezea Jangwani mara atakaporudi kwao, imefahamika.


Hiyo ni siku chache tangu uongozi wa Yanga utangaze kumuacha mshambuliaji huyo na kumsajili mwingine Mbrazili, Emerson De Oliveira, 24, anayetarajiwa kutua nchini kesho Jumanne akiongozana na kocha wake, Marcio Maximo.

Mshambuliaji huyo, amefanikiwa kufunga bao moja pekee katika Ligi Kuu Bara akicheza michezo yote saba ambalo alilifunga wakati timu yake ilipocheza na Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa mshambuliaji huyo, taarifa za kuondoka kwa Jaja hazijawashtua kabisa wachezaji kutokana na kuaga kutorejea kuichezea tena Yanga mara atakaporejea kwao Brazil.

“Hizo taarifa za kutorejea kwa Jaja, mimi hazijanishtua kabisa kwa sababu kabla ya kuondoka niliwahi kukaa naye na kuniambia kuwa, mara atakaporejea kwao basi hatarudi tena kuichezea Yanga.

“Siyo mimi peke yangu kuniaga, wapo baadhi ya wachezaji ambao alikuwa nao karibu aliwaaga na sababu kubwa ikiwa ni mashabiki kuonekana kutokubali uwezo wake.


“Mashabiki walikuwa wakimpa presha akiwa ndani na nje uwanja, amekuwa akikosa amani kabisa hali iliyomfanya ashindwe kucheza soka, hivyo akaona ni bora asirudi tena na badala yake aende akatafute maisha kwingine,” kilisema chanzo hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic