November 24, 2014


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu.


Malinzia amepelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu, ingawa haikuelezwa anasumbuliwa na kitu gani.

Lakini alipozungumza na gazeti hili, Malinzi amesema kweli yuko nchini India kwa ajili ya matibabu lakini ni ya kawaida kila mwaka.

“Nimekuwa nikipenda kufanya uchunguzi wa afya kila mwaka. Hivyo niko India kwa ajili ya uchunguzi wa kiafya.

“Baada ya kukamilisha kila kitu, ninatarajia kurejea nyumbani baada ya wiki siku chache kuendelea na majukumu,” alisema Malinzi.

Hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume nchini Marekani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic