November 26, 2014


Kikosi cha Rea  Madrid kina wachezaji nane ambao wameingia kwenye kuwania tuzo ya kikosi bora cha Ulaya.

Tuzo hiyo ya Uefa ya mwaka 2014 itakayotolewa hivi karibuni inajumuisha pia wachezaji wanne kutoka AtleticoMadrid ambao pia wanaiwania.

Wanaowania kuingia kwenye first eleven ya mwaka ya Uefa ni hawa.

Kutoka Madrid maarufu kama Los Blancos ni Carvajal, Ramos, Kroos, Modric, James, Bale, Benzema na Cristiano Ronaldo.

Kwa Bayern wao wana namba sawa na Real Madrid ya watu nane ambao ni Neuer, Alaba, Benatia, Boateng, Lahm, Xabi Alonso, Müller na Lewandowski.

Upande wa Atletico Madrid ambayo imetoa wachezaji wanne ni Koke, Arda, Godín na Miranda.

Wengine kutoka katika timu nyingine ni Xabi Alonso (Bayern Munich) na Di María (Manchester United), Courtois (Chelsea), Diego Costa (Chelsea).
Kwa upande wa Barcelona imetoa wachezaji watatu ambao ni Rakitic, Neymar na Messi.


Aliyewashangaza wengi kuingia katika tuzo hizo ni Jonathan Soriano (Red Bull Salzburg).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic