November 23, 2014

Bayern Munich ndiyo timu tajiri zaidi nchini Ujerumani na kama utazungumzia kwa ujumla, basi Bundesliga ndiyo ligi ghali zaidi kifedha barani Ulaya.

Ukitaka uhakikishe hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayern maarufu kama Bavarian, Karl-Heinz Rummenigge amesema wameishalipa fedha zote walizokuwa wakidaiwa kwenye uwanja wao.

Uwanja wa The Allianz Arena uliojengwa mwaka 2005, umewagharimu kitita cha euro 346 na walitakiwa kulimaliza deni hilo mwaka 2030.

Kutokana na fedha nyingi wanazoingiza, Bayern tayari wamelipa deni lote.
Hali hiyo imewashangaza wataalamu wengi wa masuala ya uchumi.

Awali uwanja huo ulikuwa ukimilikiwa kwa pamoja na Bayern na 1860 Munich,  lakini sasa Bayern inaumiliki kwa 100%.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic