KASEJA AKISAINI KUICHEZEA YANGA MBELE YA BIN KLEB (KUSHOTO) ANAYEONEKANA NYUMA NI ABDULFATAH AMBAYE SHUGHULI YA KUSAINI ILIFANYIKA OFISINI KWAKE KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM. |
Kumekuwa na malumbano ya hapa na pale katika
ya Menaja wa kipa mkongwe nchini, Juma Kaseja na uongozi wa Yanga.
Meneja huyo, Abdulfatah Saleh amekuwa
akisisitiza kuhusiana na suala la mchezaji wake kwamba hajalipwa fedha zake
kama ilivyokuwa inatakiwa.
Alieleza siku sahihi iliyotakiwa kulipwa fedha
hizo na akasisitiza kufanya hivyo ni kutotekeleza mkataba sahihi.
KASEJA AKISAINI MBELE YA SEIF MAGARI. ANAYEONEKANA NYUMBA NI ABDULFATAH |
Lakini akasisitiza suala la mchezaji wake
kupata nafasi kwa kuwa anaamini kiwango chake.
Uongozi wa Yanga ulijibu hoja hizo juujuu na
kusisitiza kwamba amelipwa lakini Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu akasema
hamtambui meneja huyo.
Njovu akasisitiza meneja huyo hatambuliki na
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) wala lile la Tanzania (TFF).
ABDULFATAH |
Mazungumzo hayo ya uongozi wa Yanga yanaweza
yakawa si hoja ya msingi hata kidogo labda kama Njovu atasema ana utani na
Abdulfatah kwa kuwa ni mshikaji wake.
Lakini katika ishu muhimu na makini kama hiyo,
Yanga hawapaswi kuleta utani badala yake kufanya mambo kwa uhakika na kutimiza
ahadi zao inavyotakiwa.
Wanajua hawajamlipa Kaseja, basi wana kila
sababu ya kufanya hivyo mara moja kwa kuwa viongozi ndiyo wanaopaswa kuwa
watetezi wa wachezaji.
Njovu ndiye mtendaji, hapaswi kuacha mianya
ndani ya Yanga, kikubwa amalizane na Kaseja na kupunguza malumbano hayo. Si lahisi
meneja wa Kaseja atakurupuka na kuanza kudai mchezaji wake alipwe wakati malipo
yaliishafanyika.
Lakini kusema hawamtambui meneja huyo ni jambo
jingine la kuchekesha pia. Kama mwenye alivyosema, wakati Kaseja anajiunga na
Yanga, alisaini fomu za usajili ofisini kwake.
Ukiziangalia hizo picha Abdulfatah anaonekana
nyuma wakati Kaseja akisaini mbele ya mabosi wa Yanga Seif Ahmed ‘Magari’ na
Abdallah Bin Kleb.
Maana yake, Abdulfatah ndiye alisimamia mchezo
mzima na Yanga wanamtambua. Kama wangekuwa hawamtambui, wasingefika ofisini
wake, wasingefanya shughuli ya kusaini ofisini kwake. Hivyo Yanga mjibu hoja za
msingi na ikiwezekana mlimalize suala hili kuliko kutaka kulizungusha na mwisho
kulikuza.
0 COMMENTS:
Post a Comment