November 21, 2014


Mbio za usajili wa dirisha dogo zinaendelea, Simba, Yanga na Azam ndizo zinazotajwa kwa wingi katika mbio hizo za usajili, beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani ameamua kufunguka kuhusu uwezekano wa yeye kurejea kuichezea timu yake ya zamani, Simba.


Yondani amefunguka kuwa, licha ya kuwa Simba imekuwa ikihaha kutafuta beki wa kati, yeye hana mpango wa kuihama Yanga kwa sasa na anachowaza ni kuelekeza nguvu na akili yake kuipa mafanikio timu yake.

Kauli hiyo imekuja licha ya kuwa hivi karibuni, Kocha wa Simba, Patrick Phiri, alitamka wazi kuwa anatamani kusajili beki wa kati.

Yondani ambaye amewahi kufanya kazi na Phiri, amesema kitendo cha kubadilisha timu kila wakati kwa kuhamahama hakileti picha nzuri kwa mashabiki, hivyo haoni sababu ya kuondoka na badala yake atabaki kuitumikia Yanga kwa muda mrefu.

“Kiukweli kabisa timu hizi za ligi kuu haswa hizi za Simba na Yanga, hazina utofauti wowote, mwisho wa siku utazunguka, maisha hayatabadilika.

“Mimi nimepanga kubaki kuendelea kuichezea Yanga katika kipindi chote nitakachocheza soka, nimechoka na hamahama za klabu za hapa nchini, labda niende nje ya nchi katika kutafuta mafanikio.

“Najua hilo la kwenda kucheza nje ya nchi ni ngumu, kwa sababu Watanzania wengi hatupendani, hatupendi kuona mwenzetu anafanikiwa katika maisha, ninaamini nina kiwango kikubwa cha kucheza soka, nikuhakikishie kuwa mimi ni beki bora hapa nchini,” alisema Yondani.

Yondani alitokea Simba na kujiunga na Yanga, usajili uliozua gumzo kubwa katika soka Tanzania.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic