December 18, 2014


Kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amewaita mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ili waione kazi yake.


Simba itakipiga na Mwadui FC keshokutwa katika mechi ya kirafiki iliyoandaliwa kama mazoezi kwa timu zote mbili.

Kocha huyo wa Mwadui FC inayoshiriki daraja la kwanza, amesema mashabiki wa Simba waende wakaone kazi yake ili wajue yeye si mtu wa majungu, badala yake kazi.

"Nawaomba waje kwa wingi ili waone kwa macho yao, kwamba Julio ni nani. Simba wamekuwa wananifukuza na kunirudisha.

"Kweli mimi ni Simba, lakini wakati mwingine nakuwa sipendi mambo ninayofanyiwa. Mimi ni mchapakazi, nimewabadili na kuwasaidia vijana wengi wenye mafanikio leo.

"Sasa Jumamosi kila mmoja aje aone, huyu Julio ni mtu wa majungu au kazi yake vipi," alisema Julio akionyesha kujiamini.

Pamoja na kuwa kocha mkuu, kocha msaidizi katika kikosi cha Simba kwa nyakati tofauti, Julio aliwahi kuwa beki tegemeo wa Simba hadi kupewa jina la Mrema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic