December 20, 2014



Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Desemba 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, imezingatia upungufu uliopo katika utekelezaji wa matumizi ya tiketi za elektroniki.


Hivyo, Kamati hiyo imeiagiza Sekretarieti ya TFF kuwasiliana na benki ya CRDB inayoendesha mfumo huo wa matumizi ya tiketi za elektroniki kuhusu upungufu huo na kuhakikisha unafanyiwa kazi.

Tiketi hizo zimeonekana kutokuwa na mafanikio wakati wa majaribio yake.

Katika viwanja kadhaa ikiwemo Mkwakwani mjini Tanga, watu walishindwa kuingia uwanjani baada ya mashine za ukaguzi wa tiketi kuharibika.
Hali hiyo ilisababisha mashabiki waliokuwa wamejazana kwa wingi kuvunja geti na kuingia ndani.

Pia zimeonekana zimekuwa hazina ulinzi wa kutosha kwani kuna baadhi ya mashabiki wa Simba walikamatwa na tiketi za wizi ambazo zilikuwa ni sahihi kabisa na zile zinaztumika.

Mashabiki hao walikamatwa katika mechi kati ya Simba dhidi Mtibwa Sugar iliyokuwa inapigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic