December 20, 2014

KESSY (KUSHOTO) WAKATI AKIWA MTIBWA SUGAR, HAPA ANAPAMBANA NA BEKI WA KUSHOTO WA SIMBA, MOHAMMED HUESSEIN 'TSHABALALA'.
Mlinzi wa kulia wa Simba, Hamisi Kessy, amekuwa akijituma vilivyo baada ya kujiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar kwa kuwa anataka kucheza katika kikosi cha kwanza.



Kessy amesema mazoezi ndiyo njia pekee ya kumuweka fiti na kufanya vizuri uwanjani.

"Kwa timu kama Simba, kutokana na ukubwa wake lazima utegemee ushindani mkubwa zaidi.

"Hivyo ni lazima kujituma na kufanya mazoezi ya uhakika ili kuwa katika kiwango kizuri cha kupambana ili kupata nafasi ya uhakika ya kucheza," alisema Kessy.

“Ndoto zangu ni kucheza soka la kimataifa na si vinginevyo. Naamini kusajiliwa na Simba ni moja ya hatua katika ndoto zangu na itakuwa taa ya mafanikio hayo, hivyo sijutii kujiunga nao."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic