December 18, 2014

 
KWIZERA AKIJIPUMZISHA KWA KUSOMA GAZETI LA CHAMPIONI...
Kiungo Pierre Kwizera amesema hakufurahia kuondolewa Simba, lakini kamwe hatamlaumu mtu.


Raia huyo wa Burundi amesema anarejea kwao Burundi kwenda kujipanga zaidi akiwa na imani, siku moja atatoka tena nje ya Burundi.

"Kwanza niwashukuru mashabiki wa Simba, kweli waliniunga mkono muda wote nikiwa na Simba, ni watu wazuri sana.
AKIWA MAZOEZINI SIMBA...
Sipendi kulaumu watu, sipendi kuwa na chuki na watu hata kama sikufurahia. Baada ya kupata malipo yangu, nitarejea nyumbani kujipanga.

"Ninaweza kucheza pale nyumbani kwa kuwa kuna timu ilikuwa inanihitaji, lakini najua siku moja nitatoka tena kwa kuwa ninakiamini kiwango changu," alisema Kiongera.

Kiongera ambaye ni mmoja wa viungo wakabaji wenye uwezo mzuri, aliachwa Simba ambayo ilikuwa ikitaka kuongeza beki.

Nafasi yake imechukuliwa na beki Juuko Murshid raia wa Uganda.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic