December 18, 2014


Kikosi cha Azam FC kilicho mazoezini nchini Uganda, sasa kitaacha basi lao na kurejea kwa ndege.


Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd amesema uamuzi huo umetokana na kuepusha wachezaji hao kuwa na uchovu kabla ya kuivaa Yanga Desemba 27.

Akizungumza kutoka Uganda, Jaffar amesema wameamua kufanya hivyo kwa kuwa safari ya Kampala hadi Dar es Salaam ni ndefu.

"Kweli tulikuja na basi, lakini uongozi sasa umeamua timu irudi kwa ndege ili kuepusha uchovu.

"Baada ya kufika Dar es Salaam, moja kwa moja tutaingia kambini kujiandaa na mechi hiyo dhidi ya Yanga," alisema.

Azam FC imekuwa kambini Uganda ambako imecheza mechi za kirafiki dhidi ya SC Villa na Bunamwaya au Vippers.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic