December 19, 2014


 Mshambuliaji wa Aston Villa, Darren Bent ameporwa magari yake mawili.

Gari aina ya Range Rover na Audi RS6 yameporwa na majambazi waliovamia kwake, wakavunja na kuchukua ufunguo wa gari hizo na kutoweka nazo.

Imeelezwa gari zote zinaweza kufikia kitita cha pauni 160,000 na Bent alikuwa amelala.

Kwa sasa Bent amepelekwa kwa mkopo kwenye kikosi cha Brighton and Hove Albion, ambako amecheza mechi tatu na kufunga bao moja.

Imekuwa ni tabia iliyosambaa kuhusiana na wizi wa magari.

Nyota kadhaa wamewahi kuvamiwa majumbani kwao na wizi hao ambao wanaelezwa kuwa na mtandao mkubwa unaopambana na Jeshi la Polisi la England.
Tayari kazi ya kuanza kuyasaka magari hayo imeanza kwa kasi kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic