December 16, 2014

KAIONGOZA YANGA MECHI SIBA TU ZA LIGI....SASA ANATIMUA KUREJEA KWAO BRAZIL...
Ingawa zimekuwa ni taarifa za siri kubwa, lakini uhakika unasema Kocha Marcio Maximo, amekubali kuondoka Yanga.

Mmoja wa viongozi wa kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga amesema, Maximo ataondoka nchini ndani ya siku tatu baada ya kukubaliana na uongozi.
"Si kwamba amefukuzwa, lakini ni makubaliano kwamba anaondoka.
"Ni kweli, lakini msitake kulikuza hili jambo ionekane kama tumemfukuza," aliuliza na alipotakiwa kujua mrithi ni nani, alikataa kusema.
Lakini taarifa nyingine zimeeleza Yanga inamrejesha Kocha Hans van der Pluijm.
"Suala la kocha gani tunaomba msubiri, hilo la Pluijm aliyekuambia nani, naomba mtuache kwanza," alikuwa mkali kiongozi huyo.

1 COMMENTS:

  1. :) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic