December 20, 2014


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri, ameamua kuweka wazi kuhusiana na suala la kuondoka kwa mshambuliaji Amissi Tambwe ambaye amejiunga na Yanga.


Amesema Tambwe raia wa Burundi alikosa nafasi kwenye kikosi chake, kwa kile alichosema hakuwa na uwezo wa kupambana na mabeki wenye nguvu ukimlinganisha na Elias Maguli.

Kauli ya Phiri imekuja siku chache baada ya Tambwe kusitishiwa mkataba wake Msimbazi, akidaiwa kushuka kiwango wakati alifanya  vyema enzi za Mcroatia, Zdravko Logarusic na Abdallah Kibadeni, hadi kufanikiwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

Phiri amechambua kitaalamu na kusema Tambwe ni mchezaji mzuri, lakini kilichomfanya asiwe na furaha Simba ni kukaa benchi, hivyo kuvurugika kisaikolojia na kujikuta akishindwa kutimiza majukumu yake kwa ufanisi akiwa uwanjani.

“Ukiangalia nilikuwa nikimpanga Maguli katika mechi ambazo niliamini zina mabeki wagumu kupitika, kitu ambacho Tambwe hakuweza kufanya, lakini alikuwa mzuri katika mechi zisizo na beki ngumu.


“Jambo hilo lilimfanya apoteze kujiamini na kukosa nafasi, hivyo kuathirika kisaikolojia na kujikuta akishindwa kufanya vizuri ndani ya uwanja,” alisema Phiri.

Phiri ni kati ya makocha wakongwe barani Afrika ambao wamewahi kung'ara kwenye ngazi za klabu na timu za taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic