December 20, 2014


Kocha Hans van der Pluijm ameanza kazi baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuinoa Yanga.


Pluijm ameanza kazi leo kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Loyola, rasmi akichukua nafasi yake ambayo ilichukuliwa na Marcio Maximo.

Msaidizi wa Pluijm anabaki kuwa yuleyule Charles Boniface Mkwasa ambaye alikuwa akifanya naye kazi katika miezi sita aliyoitumikia Yanga kabla ya kuondoka na kwenda Al Shaolah ya Saudi Arabia ambako walifanya kazi pamoja tena.

Tayari Yanga imemtupia rasmi virago vyake Marcio Maximo raia wa Brazil.

Maximo ameingia kwenye mkasa huo baada ya kupoteza mchezo dhidi ya watani wao Simba.

Yanga ilichapwa 2-0 na Myama katika mechi ya Bonanza la Nani Mtani Jembe.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic