December 21, 2014


Kocha Hans van der Pluijm amesisitiza atacheza soka la kushambulia.
Lakini akawaomba Wanayanga kumpa muda na kuwa na subira.

“Hata timu ninayoichukua leo, tayari ina mabadiliko makubwa. Kuna wachezaji wameondoka.

“Lakini nitawaamini waliopo na kuhakikisha tunafanya kazi yetu vizuri.
“Kuna suala la kuanza kujipanga upya na kuangalia tunafanya nini, tunahitaji nini, tubadilishe nini au tuendeleze kitu gani.

“Mimi na Charles (Boniface Mkwasa), tutapambana na tunaamini mambo yatakuwa mazuri,” alisema Pluijm.
Tayari kocha huyo ameanza kuinoa Yanga Jumamosi iliyopita baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Pluijm amechukua nafasi ya Marcio Maximo ambaye ametupiwa virago na Jangwani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic