December 21, 2014

MASAU
Kazi imekwiva, kesho kuna mechi ya kirafiki kati ya Ruvu Shooting dhidi ya timu ya daraja la kwanza ya Mwadui FC.


Lakini kivutio zaidi ni upinzani wa mechi hiyo ni maneno na mbwembwe za Msemaji wa Ruvu, Masau Bwire dhidi ya yale ya Jamhuri Kiwhelo 'Julio' ambaye ni kocha wa Mwadui FC.

Masau amesema wataifundisha soka Mwadui ya Julio kesho kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.

"Lengo ni kujipima, lakini tunataka tuwafundishe soka Mwadui FC. Tunataka kuona je, wanastahili kupanda Ligi Kuu Bara?

"Pia kuwaonyesha kazi ya ligi kuu ilivyo na namna ambavyo tumekuwa tukifanya mambo," alisema Bwire.

Lakini Julio ameendelea kusisitiza, licha ya kucheza mechi mfululizo ikiwemo ile waliyochapwa 3-1 na Simba, kesho Ruvu watakiona.

"Tunaendelea kucheza mechi mfululizo. Lengo ni kuhakikisha tunakuwa fiti zaidi na Ruvu wataona kazi yetu.
"Wasitupime kwa kufungwa na Simba au uchovu tulionao. Kipigo tu, hatutajali," alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic