December 19, 2014

Pamoja na ukimya, taarifa zinaeleza Yanga imeingia mkataba na Kocha Hans van der Pluijm kurudi aionoe.



Kocha huyo Mholanzi amekuwa nchini kwa siku tatu sasa na leo ameingia mkataba na Yanga huku msaidizi wake akiwa ni Charles Boniface Mkwasa.

Wawili hao waliiacha Yanga na kwenda kuinoa Al Shaolah FC ya Saudi Arabia ambayo hata hivyo hawakudumu.

Wakati wakiwa Saudi Arabia, Yanga ilimsaka na kumpata Marcio Maximo ambaye naye ametimuliwa na nafasi yake imechukuliwa na wao kwa mara nyingine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic