January 31, 2015


Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali, alizua jambo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar katikati ya wiki hii baada ya kugeuka nyuma wakati beki wa timu hiyo, Nassoro Masoud ‘Chollo’ alipokuwa akijiandaa kupiga penalti wakati timu yake ilipokuwa ikipambana na Mbeya City.


Simba iliyokuwa nyuma kwa mabao 2-1, ilipata penalti katika dakika ya 90 na ilitakiwa ikwamishe nyavuni ili kuiokoa timu hiyo na kipigo, haikuwa hivyo, penalti hiyo iligonga mwamba na kuokolewa na mabeki wa Mbeya City.

Wakati Chollo akijiandaa kupiga penalti hiyo, Dalali aligeuka na kuupa uwanja kisogo, huku mashabiki wa Simba wakiwa kimyaa. Baada ya Chollo kukosa, kiongozi huyo na wenzake wa Simba walijikuta wakiwa wapole na kuondoka uwanjani hapo kwa kuwa muda huohuo mwamuzi alimaliza mchezo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic