January 31, 2015


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara atakuwa mgeni rasmi kwenye fainali ya michuano ya Kombe la Taifa Wanawake kati ya Pwani na Temeke itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.


Mechi hiyo itakayoanza saa 10.15 jioni itachezeshwa na mwamuzi wa Shirikisho la SOka la Kimataifa (Fifa), Jonesia Rukyaa, na itaonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya Azam. Waamuzi wasaidizi ni Hellen Mduma, Agnes Alphonce, na Mwanahamisi Matiku wakati Kamishna ni Ingridy Kimario.

Timu za Ilala na Kigoma zitacheza mechi ya utangulizi kutafuta mshindi wa tatu kuanzia saa 8.00 mchana. Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Proin na kufanyika kwa mara ya kwanza nchini atapata kombe na sh. milioni tatu.

Makamu bingwa atapata sh. milioni mbili wakati mshindi wa tatu atapata sh. milioni moja. Kiingilio kwenye mechi hizo ni bure.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic