January 28, 2015


Timu ya African Sports ya Tanga, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, inahitaji pointi tatu tu kuweza kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao.


Kwa sasa, African Sports ndiyo vinara wa Kundi A wakiwa na pointi 41, baada ya juzi Jumatatu kuichapa Majimaji bao 1-0.

Leo Jumatano, African Sports itaumana na JKT Mlale kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na endapo ikishinda mchezo huo basi itakuwa imejikatia tiketi ya kucheza ligi kuu msimu ujao kwa kufikisha pointi 44 ambazo katika michezo iliyobaki timu za Majimaji, Friends Rangers na Lipuli zinaweza kuzifikia lakini haziwezi kuishusha African Sports kutokana na uwiano mzuri wa mabao ilionao.


Wapenzi wa soka kutoka Tanga wanatamani timu hiyo ipande ligi kuu ili washuhudie burudani iliyopotea kwa muda mrefu pindi zinapokutana timu hasimu kutoka jiji hilo za Coastal Union na African Sports.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic