January 31, 2015

MPIRA UMEKWISHA
Dk 90+3
Dk 90+2 Sserunkuma Simon anapiga shuti kali lakini Haule anadaka vizuri.



Dk 88 Simba wanamtoa Banda na nafasi yake inachukuliwa na Awadhi Juma.

Dk 82 Kessy anawatoka mabeki wa wili wa JKT na kupiga krosi safi, inaokolewa na kuwa kona, inaokolewa pia, kocna nyingine nayo inaokolewa.

Dk 81, Banda tena anawatoka mabeki watatu wa JKT lakini anashindwa kufunga akiwa katika nafasi nzuri kabisa.

Dk 74, Kanduru peke yake mbele ya lango la Simba akitazamana na Ivo anashindwa kuunganisha krosi nzuri

Dk 71, Simon Sserunkuma, yeye na kipa baada ya pasi nzuri ya Danny Sserunkuma lakini anawashangaza wengi kwa kupiga nje.


Dk 69 JKT wanamtoa Ally Bilal nafasi yake inachukuliwa na Issa Kanduru
Dk 68 Ajib anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Simon Sserunkuma

Dk 62 Ivo anataka vizuri mpira wa krosi ya Jabir Aziz
Dk 57 Banda anapewa kadi ya njano baada ya kufanya madhambi lakini inaonekana ni baada ya mwamuzi Hashim kushinikizwa na wachezaji wa JKT.
Dk 55 Okwi anawatoka mabeki wa JKT, akiwa pekee na kipa Haule anapaisha buuuuu

Dk 52 Ramadhani Shamte analambwa kadi ya njano kwa kumkata Okwi kutokea nyuma.

GOOOOOO Dk 48 Sserunkuma anafunga bao la kichwa akiunganisha basi safi ya Okwi aliyewatoka mabeki wa Ruvu.

Dk 46, JKT wanamuingiza Najib Magulu badala ya Iddi Mbaga.

MAPUMZIKO:
DK 45+3 Kessy anatoa pasi safi lakini Ajib anashindwa kuuwahi na kuwa goal kick.


Dk 45, Ajib anampiga chenga kipa JKT lakini pasi aliyompa Singano anashindwa kuitumia vizuri na JKT wanaokoa.


Dk 42, Simba inafanya shambulizi kali lakini JKT wanajitahidi kuokoa shuti kali la Banda.


Dk 38, Abdi Banda anawatoka mabeki wa JKt na kutoa pasi kwa Sserunkuma lakini mpira unaokolewa.

Dk 35, Ajibu anapiga mpira wa faulo lakini unakuwa nyanya kwa Haule

Dk 32, Kipa Haule wa JKT anadaka vizuri mpira wa kichwa na Isihaka.
Dk 29 JKT wanapata kona baada ya Tshabalala kuutoa mpira wa krosi wa Ally Bilal lakini inakuwa haina matunda.

Dk 25 Banda anapiga shuti kali linapita juu ya lango la JKT.

Dk 24 mwamuzi Hashim anampa Okwi kadi ya njano wakati akilalamika kutokana na Tshabalala kufanyiwa madhambi.
GOOOOOOOOO Dk 19 George Minja anaifungia JKT kwa mpira wa kichwa akiunganisha mpira wa kona wa jabir Aziz 'Stima'. Kipa Ivo aliwahi kutoka langoni na kuukosa mpira

Dk 17, Ivo anafanya kazi ya ziada kudaka shuti la Mgisa baada ya mabeki wa Simba kujichanganya.

Dk 13, Kamutu anapiga krosi safi kwenye lango la Simba inaokolewa na kuwa kona mbayo inaokolewa pia na kuwa mpira wa kurushwa.


Dk 8 Aziz anapata mpira mzuri kutoka kwa Kamutu na kupiga mpira mzuri lakini Ivo anaudaka kiufundi
Dk 7, Ivo Mapunda anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa faulo wa Jabir Aziz, inakuwa kona lakini isiyo na matunda.


GOOOOOO Dk 2 Danny Sserunkuma anafunga bao baada ya kuiwahi pasi ndefu ya Emmanuel Okwi.

Dk 1, Mpira unaanza kwa kuchezwa zaidi katikati ya uwanja kwa kila timu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic