January 26, 2015


Unaweza ukaona kama haiwezekani kwamba soka pia ni mchezo hatari na hilo limejidhihirisha katika mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Azam FC dhidi ya Simba.


Daktari amesema, moyo wa mshambuliaji Emmanuel Okwi ulisimama kwa sekunde kadhaa alipogongwa kisogoni na beki Aggrey Morris wa Azam FC. Maana yake kitafsiri, hiyo ni nusu kifo.


Okwi aligongwa katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC iliyomalizika kwa sara ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.

Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema moyo wa Okwi ulisimama kwa sekunde kadhaa kutokana na pigo la kisogoni karibu kabisa na ubongo katika eneo la Medullar Oblangata.

“Hakikuwa kitu kidogo, tulilazimika kufanya tiba ili kurudisha mapigo ya moyo wake. Aliumia na uliona akitoa mapovu. Ndiyo maana uliona tulikuwa tukimkandamiza kwenye kifua ili kuamsha tena mapigo yake ya moyo upya.

“Baada ya hapo, tuliona ni jambo la msingi kumfikisha Muhimbili ambako vipimo vyote vimefanyika. Imeonekana hakuumia sana na ameruhusiwa.

“Lakini mimi nimeamua kumpumzisha kwa siku mbili ili kuangalia kama atakuwa katika hali gani maana mwanzo unaweza kuona yuko vizuri kumbe kuna tatizo.

“Ikionekana anaendelea vizuri, basi ataana mazoezi lakini zoezi na atakuwa chini ya uangalizi wangu,” alisema Dk Gembe.

Mshambuliaji wa Simba, Danny Sserunkuma alitumia muda mwingi kumlaumu Morris kwamba alishiriki kumpiga Okwi kiwiko, hata hivyo alikuwa akikanusha.
Okwi alibebwa haraka na kutolewa uwanjani na baadaye kukimbizwa Muhimbili ikiwa ni baada ya kuzinduka.

Kugongwa huko kwa Okwi, jana jioni kulizua gumzo kwa mashabiki wa soka nchi hasa wa Simba ambao walikuwa wakipiga simu katika ofisi za gazeti hili wakidai mabeki wamekuwa wakatili kwa washambuliaji.

Wengi walitolea mfano wa beki George Michael wa Ruvu Shooting kumkaba mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic