January 27, 2015

MBEYA CITY WAKATI WAKITUA JANA JIJINI LEO

Mbeya City wametamba kwamba wamekuja jijini Dar es Salaam kuchukua pointi tatu.

Wakali hao wa Mbeya wametamba watachukua pointi hizo tatu katika mechi dhidi ya Simba kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Mbeya City, Dismas Tena ametamba kwamba wana nafasi ya kuchukua pointi tatu kutokana na maandalizi yao.

"Mechi zetu mbili za mwisho tumeshinda moja na sare moja. Tunaamini tuko vizuri na uhakika wa kushinda ni asilimia nyingi zaidi," alisema.

Katika mechi mbili za msimu uliopita, Simba na Mbeya City hakuna iliyokuwa imewahi kumshinda mwenzake.

Mechi ya kwanza jijini Dar es salaam, ilikuwa sare ya bao 2-2 kabla ya sare ya bao 1-1 mjini Mbeya.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic