January 30, 2015


Baada ya Simba kufungwa mabao 2-1 na Mbeya City, juzi Jumatano katika Ligi Kuu Bara, Kocha wa Simba, Goran Kopunovic, amefunguka kuhusu sababu zilizochangia kipigo hicho huku akimtaja mchezaji mmoja kuhusika.


Kocha huyo raia wa Serbia ametoa tamko juu ya mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa kwa kusema kuwa kukosekana kwa baadhi ya wachezaji wake, hasa Said Ndemla kulisababisha upungufu mkubwa kwenye nafasi ya kiungo.

Ndemla amepumzishwa kwa wiki mbili baada ya kuumia goti kwenye mechi yao dhidi ya Azam FC.

“Tumefungwa kihalali lakini kuna kitu pia nilikikosa kwenye timu yangu, Ndemla ni msaada mkubwa sana, ni mchezaji niliyemuona mapema wakati natua kuifundisha Simba, ana kila kitu kulingana na nafasi yake, kama angekuwepo sidhani kama tungepoteza kirahisi kama ilivyokuwa.

“Ndemla amebarikiwa sana, naweza kusema ni kipaji cha kipekee katika soka la Tanzania, kama akiangaliwa kwa makini anaweza kuwa faida kubwa mno kwa taifa lake, nimemkosa kwenye mechi, siwezi kusema kwamba angeitetea timu peke yake lakini angekuwa na lolote la kutusaidia katika kutafuta ushindi.

“Sina la kufanya, nitamsubiri apone lakini kila mchezaji ana ubora wake na sifa zake, naweza kuwatumia wengine lakini Ndemla atabaki kuwa Ndemla kulingana na ubora wake,” alisema Kopunovic.

Ndemla aliyetokea timu ya vijana ya Simba, amekuwa chaguo la kocha huyo na makocha wengi wanaotua kuinoa timu hiyo huku akisifika kwa kukaba, kuichezesha timu na kupiga mashuti.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic