January 26, 2015


Hali ya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi sasa iko safi kabisa na anatarajia kuanza mazoezi kesho.


Okwi alizimia na kukimbizwa hospitali jana wakati Simba ikimenyana na Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Daktari wa Simba, Dk Gembe amesema Okwi sasa yuko vizuri na kesho ataanza mazoezi taratibu.

"Niliona siku mbili zingemtosha lakini leo nimemuangalia naona yuko katika hali nzuri kabisa.

"Kesho ataanza mazoezi kidogokidogo na baada ya hapo nitamuangalia tena," alisema Dk Gembe.

Beki wa Azam FC, Aggrey Morris ndiye amekuwa akituhumiwa kumpiga kiwiko Okwi.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic