January 30, 2015

OKWI (WA PILI KUSHOTO KATIKA MSITARI WA MBELE) AKIJIFUA NA WACHEZAJI WENZAKE WA SIMBA KWENYE UWANJA WA KAMBI YA JESHI YA DEGE JIJINI DAR ES SALAAM, LEO.

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amefanya mazoezi na timu yake leo katika kambi ya Jeshi ya Dege Beach jijini Dar es Salaam.


Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema kwa hali aliyonayo, uhakika atamtumia katika mechi ya kesho dhidi ya Ruvu JKT.

"Kama ulivyomuona, sasa anaonekana yuko fiti na amefanya mazoezi vizuri. Sasa tusubiri kesho tutaamkaje lakini suala la kucheza linaonekana halina shida kwake," alisema Kopunovic.

Tayari kocha huyo amekaa na wachezaji wake na kuzungumza nao kuhusiana na makosa yaliyojitokza na marekebisho waliyofanya.

Okwi aliumia katika mechi dhidi ya Azam FC na ilielezwa alipigwa kiwiko na beki wa Azam Aggrey Morris hali iliyosababisha akose mechi iliyopita dhidi ya Mbeya City.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic