January 26, 2015

Mwanamasumbwi maarufu duniani, Manny Pacquiao ameonyesha ana kipaji hata cha kuchagua warembo bomba.


Alifanya hivyo wakati wa mashindano ya Miss Universe usiku wa kuamkia leo.

Mkali huyo wa masumbwi alikuwa mmoja wa majaji akishirikiana na bilionea Donald Trump na mtangazaji maarufu wa vipindi vya runinga Kristin Cavallari.


Majaji hao akiwemo Pacquiao walimpa ushindi Miss Colombia Paulina Vega.


Kwa mwaka jana pekee, Pacquiao kutokea Ufilipino aliingiza kitita cha paini milioni 200 katika mapambano yake ya ngumi za kulipwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic