January 30, 2015


Salata la mshambuliaji wa Simba, Elius Maguri kufanyiwa vitendo vya udhalilishwaji vimepingwa kwa nguvu zote na uongozi wa Simba.

Rais wa klabu hiyo, Evans Elieza Aveva kitendo alichokifanya beki Juma Nyosso dhidi ya Maguri kumshika makalio na kumdhalilisha kwa kumuingiza kidole lilikuwa jambo si la kiungwana.
Nyosso alifanya kitendo hicho cha kulaaniwa katika mechi ya  Ligi Kuu Bara Kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar.

Gazeti maarufu la michezo nchini la Championi, limechapisha picha ikimuonyesha Nyosso akifanya vitendo hivyo vya udhalilishaji dhidi ya Maguri, kitu ambacho wadau wengi wamelaani na kusema Nyosso hakustahili kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, Aveva alisema Maguri ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea Ruvu Shooting, alifanyiwa kitendo cha udhalilishaji na kuitaka TFF kuchukua hatua za kisheria dhidi kwa Nyosso aliyewahi kuichezewa Simba.



“Kuhusiana na suala la tukio hilo kuchapishwa kwenye gazeti la Championi kwamba ni sawa au la, kitaaluma mimi si mtaalamu wa masuala ya habari, lakini tutalijadili na wenzangu.

“Lakini la msingi ninaloweza kusema ni kwamba kitendo alichofanyiwa Maguri si sawa kabisa na tunakikemea vikali, kwani tumesikitishwa sana.

“Pia hii ni changamoto wa viongozi wa klabu na shirikisho. Kwamba huu ndiyo wakati wa kwenda na teknolojia. Tusikatae kw akuwa mambo ndivyo yalivyo.

“Angalia suala la Suarez alipomng’ata  mchezaji wa Italia, Fifa ilimfungia baada ya kutumia teknolojia na haikutumia ripoti ya waamuzi pekee, hivyo na sisi umefika wakati wa kuheshimu teknolojia kwa ajili ya kukomesha vitendo kama hivyo ambavyo tayari vimejionyesha kwa Tambwe, Okwi na Maguri, lakini pia huko daraja la kwanza ndiyo usiseme,” alisema Aveva.


Aidha, Aveva alivishukuru vyombo vya habari kwa kuendelea kuibua mfululizo matukio mabaya ya ukatili na udhalilishaji katika soka ili kuonyesha hali halisi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic