January 27, 2015

KATIBU MKUU WA SIMBA, STEPHEN ALLY (KATIKATI) AKIWAONYESHA WAANDISHI WA HABARI KIPANDE CHA MECHI HIYO. KUSHOTO NI MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI, IDDI KAJUNA NA MSEMAJI HUMPREY NYASIO.
Uongozi wa Simba umeonyesha marudio ya mechi kati ya Simba dhidi ya Azam FC na namna beki Aggrey Morris alivyompiga kiwiko mshambuliaji Emmanuel Okwi.



Okwi alianguka na kuzimia baada ya kuelezwa kuwa aligongwa nyuma ya kichwa na Morris. Okwi alilazimika kukimbizhwa hospitali na jambo hilo limekuwa likizua utata.

Katibu Mkuu wa Simba, Stephen Ally ameonyesha sehemu hiyo ya mchezo mbele ya waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo na kusema wamefungua mashitaka kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Sehemu ya picha hiyo imeonyesha namna Okwi alivyogongwa nyuma ya kichwa na kuanguka wakati faulo ikipigwa.

"Tayari tumewasilisha barua TFF tukitaka hatua zichukuliwe kwa Morris kutokana na kitendo hicho cha kikatili.

"Lakini pia tumewaeleza kwamba waamuzi hao wanapaswa kufungiwa kwa kuwa hawakuchukua hatua yoyote.

"Utaona hata mwamuzi mchezo ulimshinda, alishindwa kutoa adhabu katika matukio lukuki kuhusia na namna wachezaji wa Azam FC walivyokuwa wakivuruga mchezo," alisema Ally.

"Hali halisi ndiyo hiyo, tunalaani kwa nguvu zote vitendo hivyo vya udhalilishaji,"aliongeza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic